Mwanamke angali tata katika ushairi wa kisasa?

Sanaa ya ushairi inajisawiri kama nyenzo muhimu katika maendeleo na ukuaji wa binadamu ulimwenguni. Ujenzi wa taswira zinazowasilisha mada nyeti za kijamii ni changamoto ya kiusanii inayoibua maswala tata. Ndiposa wasilisho hili linachunguza mjadala wa usawiri wa mwanamke katika ushairi wa kisasa. M...

Full description

Bibliographic Details
Main Author: Indede, Florence
Other Authors: Chuo Kikuu cha Maseno, Idara ya Kiswahili na Lugha Nyingine za Kiafrika
Format: Article
Language:swh
Published: Universitätsbibliothek Leipzig 2012
Subjects:
Online Access:http://nbn-resolving.de/urn:nbn:de:bsz:15-qucosa-98382
http://nbn-resolving.de/urn:nbn:de:bsz:15-qucosa-98382
http://www.qucosa.de/fileadmin/data/qucosa/documents/9838/18_10_Indede.pdf
Description
Summary:Sanaa ya ushairi inajisawiri kama nyenzo muhimu katika maendeleo na ukuaji wa binadamu ulimwenguni. Ujenzi wa taswira zinazowasilisha mada nyeti za kijamii ni changamoto ya kiusanii inayoibua maswala tata. Ndiposa wasilisho hili linachunguza mjadala wa usawiri wa mwanamke katika ushairi wa kisasa. Mada nyingi zinazohakiki matini za kishairi hulenga miuundo, mitindo na maswala mengineyo ya kijamii bila kuangazia swala la utata wa mwanamke. Uzingatifu wa vipengee hivi umefifisha uangafu wa taswira ya mwanamke katika ushairi wa Kiswahili kana kwamba ushairi umempuuza mwanamke kama mhusika mkuu. Tunachukulia kwamba matini za kishairi za kisasa zinahusisha mbinu na nyenzo mpya ambazo zimebadilisha sura na taswira ya mwanamke. Maswali yanayoibuka ni; Je, Mwanamke angali tata katika ushairi wa kisasa kwenye enzi ya karne ya ishirini na moja? Je, umbo jipya la mwanamke ni lipi katika ushairi wa kisasa?